Hondohondo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bycanistes)
Hondohondo
Hondohondo rangi-mbili
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Bucerotidae (Ndege walio na mnasaba na hondohondo)
Rafinesque, 1815
Ngazi za chini

Jenasi 15:

Hondohondo (pia hondo) ni ndege wakubwa wa familia Bucerotidae. Spishi ndogo zinaitwa fimbi kwa kawaida. Wana domo kubwa na lile la spishi nyingi lina aina ya pembe juu lake. Domo linaweza kuwa jeusi, jeupe, jekundu au njano. Ndege hawa hula matunda, wadudu na wanyama wadogo. Spishi za msitu hula matunda hasa na zile za nyika hula wadudu na wanyama zaidi.

Jike wa hondohondo huyataga mayai 2-6 katika tundu ndani ya mti au pengine katika tundu la kigong'ota au zuwakulu. Dume afunga mwingilio wa tundu kwa matope, mavi na nyama ya matunda. Awaletea jike na makinda chakula.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]