By The Tree

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
By The Tree
By The Tree wakiwa wameshinda tuzo za Dove.
By The Tree wakiwa wameshinda tuzo za Dove.
Maelezo ya awali
Asili yake Weatherford, Texas
Aina ya muziki Kikristo
Nyimbo za Kikristo za Kisasa
Kazi yake Wanamuziki
Miaka ya kazi 1997 hadi sasa
Studio Fervent Records
Wanachama wa sasa
Aaron Blanton
Ben Davis
Dustin Sauder
Eric Green


By The Tree ni kundi la muziki wa Kikristo la kisasa lililoshinda tuzo ya Dove mara mbili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

By The Tree ilianzishwa katika Weatherford, Texas katika mwaka wa 1997 na Chuck Dennie na Bala Boyd.

Kama makundi mengi ya muziki, By The Tree walipata kuanza kazi yao kwa kuimba katika matukio madogomadogo - hasa katika makanisa - kote kusini na kusini magharibi wa Marekani. Kusafiri kwao na kufanya ziara mbalimbali kulikuza umati za mashabiki.

Katika mwaka wa 1999,walitoa albamu mbili za kujitegemea(bila kuwa na udhamini wa studio yoyote) ,wakarekodi wenyewe na wakaziuza katika matamasha yao na matukio waliohudhuria. Ilipofika mwaka wa 2001, 30,000 za albamu hizi zilikuwa zimeuzwa.Hii ilileta faida kubwa zaidi ya hela walizotumia kurekodi nyimbo hizo.Aidha ya hayo, iliwafanya wajulikane katika sekta ya nyimbo za Kikristo.

Hatimaye,bendi ilitia saini mkataba na Fervent Records, sehemu ya kampuni ya muziki ya BMG.. Albamu yao ya kwanza iliyorekodiwa ya kitaifa ilikuwa Invade My Soul. Albamu hii ilikuwa katika chati ya nyimbo bora 40 ya Billboard katika sehemu za nyimbo za kisasa na vile vile sehemu ya huru au kujitegemea. Albamu hii ilishinda tuzo mbili za Dove.Albamu yenyewe ikishinda tuzo ya Albamu Bora katika aina ya muziki ya Rock/Alternative na wimbo wa albamu ukishinda tuzo ya Nyimbo Bora Uliorekodiwa.

Bendi hili limebadilika mara kadhaa tangu kutia saini mkataba na Fervent huku wanachama wengine wakiongezeka na wengine kutolewa. Mwimbaji na mchezaji gitaa ,Aaron Blanton aliungana na kundi hilo kabla ya kurekodi kwa Invade My Soul na Samuel McKern(mchezaji ngoma) akiondoka. Chuck Dennie alikuwa mwimbaji kiongozi na mchezaji gitaa hadi mwaka wa 2005. Ben Davis alijiunga nao katika mwaka wa 2002 kwa ajili ya kurekodi These Days. Mwanachama wa hapo awali wakianza,Kevin Rhoads,aliondoka muda mfupi kabla ya kutolewa kwa These Days na nafasi yake kuchukuliwa na Charlie Goddard (aliyeondoka bendi katika mwaka wa 2003 kuungana na bendi la Jeff Deyo).

By The Tree imetoa albamu nne likiwa na Fervent Records na wao ni kundi maarufu katika muziki ya Kikristo ya kisasa.

Chuck Dennie sasa anaishi Edmond,OK na mke wake Joanne na ni mfanyikazi katika kanisa lenye kampasi mbalimbali linalojulikana kama LifeChurch.tv kama mchungaji wa kuabudu katika kampasi ya Kaskazini Magharibi wa OKC.

Wanachama wa sasa[hariri | hariri chanzo]

  • Aaron Blanton (mwimbaji/mchezaji gitaa)
  • Ben Davis (piano/mwimbaji)
  • Dustin Sauder (kiongozi wa kucheza gitaa/mwimbaji)
  • Eric Green (mchezaji ngoma)

Wanachama wa zamani[hariri | hariri chanzo]

  • Cameron Tucker – (Alishiriki katika "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
  • David Canington – piano (Alishiriki "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
  • Betsy Caswell –mwimbaji(Alishiriki "Passion For Jesus '99" na "Shoot Me Down")
  • Kevin Rhoads – mwimbaji, mchezaji gitaa
  • Samuel McKern – mchezaji ngoma
  • Charlie Goddard – mwimbaji,mchezaji gitaa
  • Rocky Presley –
  • Chuck Dennie – mwimbaji,mchezaji gitaa
  • Garrett Goodwin – mchezaji ngoma
  • Dan Castillo – mchezaji gitaa ya bass
  • James Putnam – mchezaji gitaa ya bass
  • Melissa Stein – mwimbaji

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

  • Passion For Jesus (1999) Walirekodi na kusambaza wenyewe
  • Shoot Me Down (1999) Walirekodi nakusambaza wenyewe
  • Invade My Soul (Fervent Records, 2001) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #35
  • These Days (Fervent, 2002) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #17
  • Root (Fervent, 2003) Nambari katika chati ya Marekani ya Kikristo #15
  • Hold You High (Fervent, 2004)
  • World On Fire (Fervent, 2006)
  • Beautiful One: The Best of By The Tree (Fervent, 2007)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [1]
  2. [2]
  3. [3]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu By The Tree kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.