Butiama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Butiama
Butiama is located in Tanzania
Butiama
Butiama
Mahali pa mji wa Butiama katika Tanzania
Anwani ya kijiografia: 1°46′12″S 33°58′12″E / 1.77°S 33.97°E / -1.77; 33.97
Nchi Tanzania
Mkoa Mara
Wilaya Musoma vijijini
Idadi ya wakazi
 - Mji 15,383
Nyumba ya kaburi la Mwalimu Nyerere katika kijiji cha Butiama

Butiama ni mji ulio makao makuu ya wilaya ya Butiama katika Mkoa wa Mara (Tanzania). Uko karibu na Ziwa Viktoria.

Wenyeji asilia ni kabila la Wazanaki. Wakati wa sensa ya 2002 idadi ya wakazi wa kata ya Butiama ilikuwa 15,383. [1]

Wilaya hiyo ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012.

Butiama imejulikana kimataifa kwa sababu ni mahali ambako alizaliwa rais wa kwanza wa Tanganyika halafu wa Tanzania Julius Nyerere. Aliendelea kuwa na nyumba kijijini alikorudi baada ya kustaafu kama rais na baadaye pia kama mwenyekiti wa chama tawala cha CCM. Baada ya kufariki kwake (London 14 Oktoba 1999), makazi yake yamekuwa nyumba ya makumbusho. Pia nyumba ya kaburi lake iko katika kijiji cha Butiama.

Kuna pia meli inayoitwa "Butiama" inayozunguka ziwani kati ya Mwanza na Ukerewe.

Marejeo [hariri]

  1. 2002 Population and Housing Census General Report Musoma rural (en). Government of Tanzania.
Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Butiama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.