Busagara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Busagara ni kata ya Wilaya ya Kibondo katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania.

Vijiji[hariri | hariri chanzo]

Busagara ni kata iliyopo katika tarafa ya Kifura. Kata ina vijiji 4: Kifura, Kigendeka, Kasaka na Nyaruyoba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa Busagara kilikuwa kijiji kilichokaliwa na Waha wa mdyank'o (kaya) wa Washubhi na ilikuwa moja kati ya himaya ya mwami Luhaga aliyeitawala Kibondo yote.

Baada ya uhuru mwaka 1961 wakazi walitakiwa kuishi katika vijiji vya ujamaa: ndipo walipoanzisha kijiji cha Kasanda ambacho kwa sasa kinajulikana kama Kifura; eneo ambao lililokuwa kijiji cha zamani cha Busagara kwa sasa ni mashamba.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,341 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 30,722 waishio humo.[2]

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa Busagara ni wakulima hasa wa mazao ya chakula kama vile mahindi, mihogo, maharage ya njano, mtama, karanga, magimbi n.k. Kilimo kinafanyika katika mashamba ya Kunk'ubha, Mrutunhu, Busagara, Mkugwa, Kihivfu nyensato n.k. Asilimia kubwa ya wakazi ni maskini.

Shule[hariri | hariri chanzo]

Kata ina shule za sekondari mbili: Moyowosi na Busagara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kibondo - Mkoa wa Kigoma - Tanzania

Bitare | Biturana | Bunyanbo | Busagara | Busunzu | Itaba | Kagezi | Kibondo Mjini | Kitahana | Kizazi | Kumsenga | Kumwambu | Mabamba | Misezero | Mukabuye | Murungu | Nyaruyoba | Rugongwe | Rusohoko

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Busagara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.