Bukoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bukoli ni kata ya Wilaya ya Geita katika Mkoa wa Geita, Tanzania. Msimbo wa posta ni 30121.[1]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 22,442 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 16,345 waishio humo.[3]

Hali wa maisha[hariri | hariri chanzo]

Bukoli ni mji mzuri kwa hali ya hewa iliyotulia na wakazi wake wana ushirikiano mkubwa katika masuala ya kijamii.

Gharama za maisha ziko chini ukilinganisha na mahali kama Nyarugusu, Geita Mjini, kwani wakazi wengi wa Bukoli ni wakulima. Wanalitumia vizuri daraja lisilokauka mwaka mzima kulima bustani na mazao yakomaayo mapema kwa wingi, hivyo upatikanaji wa chakula kwa bei nafuu.

Katika mji wa Bukoli kuna shughuli mbalimbali za uchumi kama jineri ya kusafisha mbegu za pamba kwa ajili ya kutoa mafuta. Jineri hizo huufanya mji wa Bukoli kuchangamka na wakazi wake kupata ajira kwa urahisi.

Bukoli Sekondari[hariri | hariri chanzo]

Katika mji huo kuna sekondari moja, iitwayo Bukoli Secondary School. Shule hii imefanya vizuri katika mitihani ya taifa kwa miaka sasa. Imekuwa kama shule mzazi kwa shule kama Nyarugusu Sekondari, Kamena Sekondari, Ntono Sekondari, Nyaruyeye Sekondari, Butobela Sekondari.

Bukoli Sekondari ilianza rasmi mwaka 1993 kama shule ya wazazi. Baada ya kuchukuliwa na serikali wanafunzi wakaanza kwenda kidato cha tano katika shule mbalimbali, kutokana na serikali kuleta waalimu waliodhamiria kufundisha kwa nguvu na kujitoa kwa moyo wote. Hii ni changamoto kwa vijana wanaosoma shule hiyo kuongeza bidii ili kufanya vizuri zaidi. kwani waliofaulu kwenda kidato cha tano na sita wote walifika vyuo vikuu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01. 
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 225
  3. Sensa ya 2012, Geita Region – Geita District Council
Kata za Wilaya ya Geita Vijijini - Mkoa wa Geita - Tanzania

Bugalama | Bugulula | Bujula | Bukoli | Bukondo | Busanda | Butobela | Butundwe | Chigunga | Isulwabutundwe | Izumacheli | Kagu | Kakubilo | Kamena | Kamhanga | Kaseme | Katoma | Katoro | Lubanga | Ludete | Lwenzera | Magenge | Nkome | Nyachiluluma | Nyakagomba | Nyakamwaga | Nyalwanzaja | Nyamalimbe | Nyamboge | Nyamigota | Nyamwilolelwa | Nyarugusu | Nyaruyeye | Nyawilimilwa | Nzera | Rwamgasa | Senga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Geita bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.