Bukabwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bukabwa ni kata ya Wilaya ya Butiama katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31205.

Kata hiyo inajumuisha vijiji vya Bukabwa yalipo makao makuu ya kata, Mmazami na Kirumi.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 13,765 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,002 waishio humo[2], kwa mchanganuo ufuatao: kijiji cha Bukabwa wakazi wapatao 3,127, kijiji cha Kirumi wakazi 3,291 na kijiji cha Mmazami wakazi 4,584.

Idadi kubwa ya wakazi ni wa kabila la Wakabwa, na kiasi kidogo jamii ya Wazanaki, Wakiroba na Wasimbiti.

Mwaka wa 2014 kijiji cha Bukabwa kilipata umeme kupitia mradi wa umeme vijijini unaodhaminia na serikali ya Tanzania kupitia wakala wa umeme vijijini (Rural energy Agent-REA).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Butiama - Mkoa wa Mara - Tanzania

Bisumwa | Buhemba | Bukabwa | Buruma | Busegwe | Buswahili | Butiama | Butuguri | Bwiregi | Kamumegi | Kukirango | Kyanyari | Masaba | Mirwa | Muriaza | Nyamimange | Nyankanga | Sirorisimba


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bukabwa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.