Bob Marley & The Wailers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bob Marley & The Wailers

Maelezo ya awali
Asili yake Kingston, Jamaica
Aina ya muziki Reggae, ska, rocksteady, roots reggae
Miaka ya kazi 1963–1981
Studio Island, Tuff Gong, Trojan, Studio One, Beverley's
Ame/Wameshirikiana na The Wailers Band, The Original Wailers, The Upsetters, I Threes
Wanachama wa zamani
Bob Marley
Peter Tosh
Bunny Wailer
Cherry Smith
Beverley Kelso
Junior Braithwaite
Constantine Walker
Hugh Malcolm
Aston Barrett
Carlton Barrett
Earl Lindo
Alvin Patterson
Rita Marley
Marcia Griffiths
Judy Mowatt
Al Anderson
Tyrone Downie
Junior Marvin


Bob Marley & The Wailers lilikuwa kundi la muziki wa reggae kutoka nchini Jamaika. Bendi ilianzishwa na Bob Marley. Kundi liliundwa wakati mwanamuziki aliyejifunza mwenye Hubert Winston McIntosh (Peter Tosh) alivyokutana na Neville Livingston (Bunny Wailer), na Robert Nesta Marley (Bob Marley) mnamo mwaka wa 1963 na kuwafunza namna ya kupiga gitaa, vinanda, na tumba.

Mwishoni mwa miaka ya 1963 Junior Braithwaite, Beverley Kelso, na Cherry Smith wakajiunga na The Wailers. Baada ya Peter Tosh na Bunny Wailer kuondoka katika bendi mnamo 1974, Bob Marley akaanza kufanya ziara na wanachama wapya wa bendi. Waitikiaji wake wapya walikuwa ni pamoja na kina ndugu Carlton na Aston "Family Man" Barrett katika upande wa magoma na besi kwa ujumla, Junior Marvin na Al Anderson walipiga gitaa, Tyrone Downie na Earl "Wya" Lindo upande wa vinanda, na Alvin "Seeco" Patterson katika upande wa tumba. Kina "I Threes", ikiunganishwa na Judy Mowatt, Marcia Griffiths, na mke wa Marley, Rita, walisaidia upande wa sauti za uitikiaji kwa nyuma.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kundi liliundwa wakati mwanamuziki aliyejifunza mwenye Hubert Winston McIntosh (Peter Tosh) alivyokutana na Neville Livingston (Bunny Wailer), na Robert Nesta Marley (Bob Marley) mnamo mwaka wa 1963 na kuwafunza namna ya kupiga gitaa, vinanda, na tumba.

Awali walifahamika kwa majina tofauti-tofauti kama vile The Teenagers, The Wailing Rudeboys, The Wailing Wailers mwisho kabisa The Wailers. Mwaka wa 1966 Braithwaite, Kelso na Smith wakaondoka katika bendi, ambapo wakabaki mtu tatu Livingston, Marley na Tosh (Neville Livingston huwa jina la kuzaliwa la Bunny Wailer).

Miongoni mwa nyimbo kali za The Wailers zilirekodiwa na Lee "Scratch" Perry na bendi yake ya studio The Upsetters. Mwanzoni mwa miaka ya 1970 wanachama wa The Upsetters Aston "Family Man" Barrett na kaka'ke Carlton (Carlie) Barrett,[1] wakaanzisha Wailers Band, wanatoa ala tupu za kusaidia The Wailers. The Wailers wamepata kurekodi kazi kadhaa za reggae na ska kama vile "Simmer Down", "Trenchtown Rock", "Nice Time", "War", "Stir It Up" na "Get Up, Stand Up".

The Wailers waliachana mnamo mwaka wa 1974 baada ya Tosh na Livingston kukataa kufanya ziara ya muziki. Bob Marley akaanzisha Bob Marley & The Wailers akiwa yeye mwenyewe mpiga gitaa, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji mkuu, kundi la Wailers Band wakiwa kama wasaidizi, na kina I Threes wakiwa kama waitikiaji. The Wailers Band wakiwa pamoja na kina Carlton Barrett na "Family Man" Barrett katika upande wa ngoma na besi, Junior Marvin na Al Anderson wakipiga solo gitaa, Tyrone Downie na Earl "Wya" Lindo wanapiga kinanda, na Alvin "Seeco" Patterson anapiga tumba. The I Threes inaunganishwa na mke wa Bob Marley Rita Marley, Judy Mowatt na Marcia Griffiths.

Wanachama[hariri | hariri chanzo]

Bob Marley & The Wailers timeline

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Lee Scratch Perry Interview, New Musical Express, 17 Novemba 1984

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]