Bob Dylan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bob Dylan jukwaani, 1996

Bob Dylan ni mwanamuziki, mwimbaji na mwandishi wa Marekani. Alikuwa anapiga muziki wa Folk na Rock. Mwaka wa 2008 alituzwa tuzo maalumu ya Tuzo ya Pulitzer ya Muziki kwa kazi ya maisha yake. Mwaka 2016 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Bob Dylan alizaliwa katika familia ya Kiyahudi kwa jina la Robert Allen Zimmerman kwenye hospitali ya St Mary's Hospital mjini Duluth, Minnesota siku ya 24 Mei 1941[1][2] . Mababu walifika Marekani kutoka Milki ya Urusi wakati wa mwanzo wa karne ya, baada ya kukimbia pogromu dhidi ya Wayahudi katika nchi hiyo.[3] Wazazi wake Abram Zimmerman na Beatrice "Beatty" Stone waliishi Duluth wakahamia baadaye mjini Hibbing. Hapo Robert alipata elimu yake akianza kupiga muziki alipokuwa mwanafunzi wa shule bado.

Mwaka 1959 alihamia Minneapolis akajiandikisha kwenye somo la sanaa na muziki ingawa hajasoma hali halisi. Badala yake alianza kucheza muziki katika klabu ya "Ten O'Clock Scholar" katika mtaa wa Dinkytown. Wakati ule alianza kutumia jina la Bob (kifupi cha Robert) Dylan kwa sababu alivutwa sana na ayat za mshairi Dylan Thomas[4]. Hapa alishawishwa pia na muziki ya Folk ya Pete Seeger, The Kingston Trio na Woody Guthrie

Ilhali kama kijana alikuwa alianza muziki ya Rock aliamua kuhamia kwenda Folk kwa sababu hakuridhika na nafasi ya matini kwenye Rock. Mapokeo ya Folk ikampa nafasi ya kusimulia hadithi na shairi kwa muziki. Alisema "Rock'n'roll kwangu haikutosha. Ina mipigo ya kuvutia lakini uimbaji wake si kamili hauwezi kutaja maisha kwa njia halisi. Nikatambua nikiingia katika muziki ya Folk, napata kitu halisi zaidi. Nyimbo zake zinajaa zaidi tamaa, huzuni, furaha, imani, hisia..."[5]


WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bob Dylan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Sounes, p. 14
  2. Robert Allen Zimmerman. Minnesota Birth Index, 1935–2002. Ancestry.com. Iliwekwa mnamo September 6, 2011. “Name: Robert Allen Zimmerman; Birth Date: May 24, 1941; Birth County: Saint Louis; Father: Abram H. Zimmerman; Mother: Beatrice Stone”Kigezo:Subscription required
  3. Sounes, pp. 12–13.
  4. Dylan, pp. 78–79.
  5. "The thing about rock'n'roll is that for me anyway it wasn't enough... There were great catch-phrases and driving pulse rhythms... but the songs weren't serious or didn't reflect life in a realistic way. I knew that when I got into folk music, it was more of a serious type of thing. The songs are filled with more despair, more sadness, more triumph, more faith in the supernatural, much deeper feelings."; taz. Crowe-1985/>