Blandina wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Blandina (kwa Kifaransa: Blandine), aliyeuawa Lyon mwaka 177 katika dhuluma wa kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo, anaheshimiwa kama mtakatifu bikira na mfiadini.

Barua iliyotufikia kutoka kwa walionusurika kuuawa wakati huo inaleta ripoti kali lakini sahihi ya mauaji hayo ya wafiadini wa Lyon yaliyofanyika katika mji mkuu wa Gallia.