Birgita wa Sweden

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Brigita akiwa amevaa kanzu na taji la shirika lake.

Birgita wa Uswidi (Finsta, Uswidi, 3 Juni 1303Roma, Italia, 23 Julai 1373) alikuwa Mkristo wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko, halafu mwanzilishi wa shirika la Mwokozi Mtakatifu.

Alitangazwa mtakatifu na Papa Bonifasi IX mwaka 1391, halafu msimamizi mmojawapo wa Ulaya na Papa Yohane Paulo II mwaka 1999.

Yaliyomo

[hariri] Maisha ya awali

Birgita alizaliwa huko Finsta, katika mkoa wa Uppland (Uswidi), katika familia ya masharifu.

Sehemu ya kwanza ya maisha yake ni ya mke mwenye watoto 8, ambao wa pili kati yao anaheshimiwa pia kama mtakatifu Katerina wa Uswidi. Pamoja na mume wake, sharifu Ulf Gudmarsson, alisoma Biblia, alianzisha hospitali na kuhudumia maskini.

Kutokana na kipaji chake kama mlezi aliitwa kwenye ikulu huko Stockholm, na hatimaye alifanya hija huko Santiago wa Compostela (Hispania).

[hariri] Baada ya kufiwa

Kisha kufiwa mume wake mwaka 1344 alijisikia kuhama nchi yake ili kuanza utume mpya akahamia Roma (1349).

Baada ya kuhiji mahali pengi Italia, kati ya miaka 1371 na 1372 alitembelea Nchi Takatifu, alipojionea mahali alipoishi Yesu. Alisema kuwa huko Yerusalemu alipewa ujumbe wa Bikira Maria wa kurudi Ulaya.

Huko aliwatabiria matukio mapapa na wafalme na kuwaonya vikali kuhusu urekebisho wa maadili ya Wakristo, akidai anawasiliana na Yesu Kristo.

Kutokana na mafumbo hayo alitunga sala 15 zilizoenea sana.

[hariri] Marejeo

  • Duffy, Eamon (1992). The stripping of the altars: Traditional religion in England, c.1400 - c.1580. New Haven: Yale University Press. ISBN 978-0-300-05342-5
  • Schiller, Gertrud; Seligman, Janet (1971). Iconography of Christian Art, Vol. I: Christ's incarnation, childhood, baptism, temptation, transfiguration, works and miracles, (English trans from German). London: Lund Humphries. OCLC 59999963

[hariri] Viungo vya nje

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:CE poster

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine