Biirabo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Biirabo ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35521 [1].

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,900 waishio humo.[2]

Ni kata ambayo inajishughulisha na kilimo hasa cha kahawa kama zao kuu.

Kuna vijiji kama Kanywangonge, Katobago, Bugarama, Kihumulo, Biirabo na Kabare.

Pia kuna shule za msingi saba kama Kanywangonge, Katobago, Bugarama, Kihumulo, Biirabo pamoja na Kabare A na B.

Shule za sekondari ni pamoja na Kihumulo na Biirabo.

Vituo vya afya ni Kabare A na B pamoja na Kanywangonge.

Kanywangonge ni kijiji kinachopatikana katika kata ya Biirabo ambacho kina vitongoji vitano: Kanywangonge, Nyamiramba, Kibera, Kamushenge na Rwakaziba. Shuguli kubwa ndani ya kijiji hicho ni kilimo cha mazao ya mboga.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. Sensa ya 2012, Kagera - Muleba-District-Council
Kata za Wilaya ya Muleba - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Biirabo | Bisheke | Buganguzi | Buhangaza | Bulyakashaju | Bumbire | Bureza | Burungura | Goziba | Gwanseli | Ibuga | Ijumbi | Ikondo | Ikuza | Izigo | Kabirizi | Kagoma | Kamachumu | Karambi | Kasharunga | Kashasha | Katoke | Kerebe | Kibanga | Kikuku | Kimwani | Kishanda | Kyebitembe | Mafumbo | Magata Karutanga | Mayondwe | Mazinga | Mubunda | Muhutwe | Muleba | Mushabago | Ngenge | Nshamba | Nyakabango | Nyakatanga | Ruhanga | Rulanda | Rutoro


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Biirabo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.