Berardo mfiadini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Berardo alizaliwa Carbio, Umbria, Italia akafia dini ya Ukristo huko Morocco pamoja na Ndugu Wadogo wenzake Petro, Oto, Accursius na Adjutus.
Ndio Wafransisko wafiadini wa kwanza. Wote wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu, hasa tangu mwaka 1481 walipotangazwa na Papa Sixtus IV.
Sikukuu yao ni tarehe 16 Januari, siku ya kifodini chao mwaka 1220.
Viungo vya nje [hariri]
- (Kiitalia) Santi Berardo, Otone, Pietro, Accursio e Adiuto Protomartiri dell’Ordine dei Frati Minori
- (Kijerumani) Antonius von Padua - mentioned in the entry for Saint Anthony
- Catholic Encyclopedia article