Benedikto Yosefu Labre
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kanisa la Santa Maria ai Monti alimozikwa.
Benedikto Yosefu Labre (kwa Kifaransa Benoît-Joseph Labré) alizaliwa tarehe 25 Machi 1748 huko Amettes, Boulogne-sur-Mer, Ufaransa akafariki tarehe 17 Aprili 1783 huko Roma, Italia baada ya kuishi miaka mingi bila ya makao maalumu, akihiji makanisa mbalimbali hasa kwa ajili ya kuabudu ekaristi.
Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 20 Mei 1859, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881.
Sikukuu yake ni tarehe 16 Aprili.
Marejeo [hariri]
- Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-140-51312-4.
Viungo vya nje [hariri]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Benedikto Yosefu Labre kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |