Ubelgiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Belgium)
Ubelgiji

Ubelgiji (België kwa Kiholanzi, Belgique kwa Kifaransa na Belgien kwa Kijerumani) ni ufalme wa Ulaya ya Magharibi. Ni kati ya nchi 6 zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ambayo baadaye imekuwa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Luxemburg.

Ina pwani kwenye Bahari ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Brussels.

Historia[hariri | hariri chanzo]

"Belgii" lilikuwa jina la wakazi wa kale wa kaskazini mwa Gallia, na Gallia Belgica ilikuwa jimbo la Dola la Roma.

Wakati wa Zama za Kati maeneo yake yalikuwa chini ya Dola Takatifu la Kiroma na tangu mwaka 1477 yalitawaliwa na nasaba ya Habsburg. Watawala hao walikuwa Wakatoliki, hivyo walizuia uenezaji wa Matengenezo ya Kiprotestanti.

Hata hivyo mikoa ya kaskazini ilifaulu kwa njia ya vita kujipatia uhuru na kuanzisha Jamhuri ya Nchi za Chini (Uholanzi) tangu mwaka 1648. Mikoa iliyoendelea kuwa Ubelgiji ya baadaye ilibaki chini ya Habsburg hadi Mapinduzi ya Kifaransa na utawala wa Napoleon aliyeiingiza katika Ufaransa.

Baada ya Mkutano wa Vienna wa mwaka 1815 Ubelgiji iliunganishwa pamoja na Uholanzi kuwa sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Nchi za Chini na hapo ilikuwa sehemu ya kusini ya ufalme huo. Tofauti na sehemu za kaskazini, zilizokuwa na Waprotestanti wengi, mikoa ya Ubelgiji ilikaliwa na Wakatoliki. Tena, wenyeji wa mikoa ya kusini kabisa waliongea Kifaransa, na pia katika sehemu nyingine, ambako watu waliongea Kiholanzi, lugha ya Kifaransa ilikuwa lugha iliyopendwa na matabaka ya juu na wasomi.

Tofauti hizo za kiutamaduni zilichangia kati ya watu wa kusini hisia ya kubaguliwa na katika mapinduzi ya 1830 mikoa yao ilijitenga na Ufalme wa Muungano wa Nchi za Chini na kuanzisha ufalme mpya wa Ubelgiji.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Ubelgiji ni shirikisho la majimbo matatu:

Katika Wallonia kuna pia wilaya ambayo wakazi wanatumia hasa Kijerumani ambacho ni lugha ya tatu ya kitaifa.[2][3]

Ushindani kama si chuki kati ya makundi hayo ndilo tatizo kuu la nchi.[4][5]

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wenyeji (67.3%) wanatofautiana hasa kutokana na lugha: 59% wanaongea hasa Kiholanzi, 40% Kifaransa na 1% Kijerumani.

Wahamiaji wanaongea lugha mama zao: Kiarabu (3%), Kiitalia (2%), Kituruki (1%) n.k.

Kiingereza kinajulikana na 38% za wakazi.

Wakazi wengi ni Wakristo (63.7%), hasa wa Kanisa Katoliki (60.6%), lakini 5% tu wanashiriki ibada za kila wiki; Wakristo wengine ni Waprotestanti (2.1%) na Waorthodoksi (1.6%). Waislamu ni 7.4%. Asilimia 28 hawana dini yoyote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Leclerc, Jacques, membre associé du TLFQ (18 January 2007). Belgique • België • Belgien—Région de Bruxelles-Capitale • Brussels Hoofdstedelijk Gewest (French). L'aménagement linguistique dans le monde. Host: Trésor de la langue française au Québec (TLFQ), Université Laval, Quebec. Jalada kutoka ya awali juu ya 9 June 2007. Iliwekwa mnamo 18 June 2007. “C'est une région officiellement bilingue formant au centre du pays une enclave dans la province du Brabant flamand (Vlaams Brabant)”
    * About Belgium. Belgian Federal Public Service (ministry) / Embassy of Belgium in the Republic of Korea. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-10-02. Iliwekwa mnamo 21 June 2007. “the Brussels-Capital Region is an enclave of 162 km2 within the Flemish region.”
    * Flanders (administrative region). Microsoft Encarta Online Encyclopedia. Microsoft (2007). Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-10-31. Iliwekwa mnamo 21 June 2007. “The capital of Belgium, Brussels, is an enclave within Flanders.”
    * Van de Walle, Steven, lecturer at University of Birmingham Institute of Local Government Studies, School of Public Policy. Language Facilities in the Brussels Periphery (PDF). KULeuven—Leuvens Universitair Dienstencentrum voor Informatica en Telematica. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-10-31. Iliwekwa mnamo 21 June 2007. “Brussels is a kind of enclave within Flanders—it has no direct link with Wallonia.”
  2. The German-speaking Community at Belgium.be
  3. The German-speaking Community. The German-speaking Community. Jalada kutoka ya awali juu ya 30 May 2007. Iliwekwa mnamo 5 May 2007. The (original) version in German language (already) mentions 73,000 instead of 71,500 inhabitants.
  4. Morris, Chris. "Language dispute divides Belgium", BBC News, 13 May 2005. Retrieved on 8 May 2007. 
  5. Petermann, Simon, Professor at the University of Liège, Wallonia, Belgium—at colloquium IXe Sommet de la francophonie—Initiatives 2001—Ethique et nouvelles technologies, session 6 Cultures et langues, la place des minorités, Bayreuth (25 September 2001). Langues majoritaires, langues minoritaires, dialectes et NTIC (French). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-11-02. Iliwekwa mnamo 4 May 2007.
Katika wavuti
Vitabu
  • Arblaster, Paul (23 December 2005). A History of the Low Countries. Palgrave Essential Histories (Hardcover 312pp ed.). Palgrave Macmillan, New York. ISBN 1-4039-4827-5. 
  • Blom, J. C. H., Dutch State Institute for War Documentation, ed.; Lamberts, Emiel, Professor in Modern History KULeuven, ed.; Kennedy, James C., translator (May 1999). History of the Low Countries (Hardcover 503pp ed.). Berghahn Books, Oxford/New York. ISBN 1-57181-084-6. 
  • Cammaerts, Émile L. (1921) [1913]. A History of Belgium from the Roman Invasion to the Present Day (357pp ed.). D. Appleton and Co, New York. ASIN B00085PM0A. OCLC 1525559. 
    [Also editions [1913], London, OCLC 29072911; (1921) D. Unwin and Co., New York OCLC 9625246 also published (1921) as Belgium from the Roman invasion to the present day, The Story of the nations, 67, T. Fisher Unwin, London, OCLC 2986704]
  • de Kavanagh Boulger, Demetrius C. (28 June 2001) [1902]. The History of Belgium: Part 1. Cæsar to Waterloo. Elibron Classics (Paperback 493pp ed.). Adamant Media (Delaware corporation), Boston, Massachusetts, United States. ISBN 1-4021-6714-8.  Facsimile reprint of a 1902 edition by the author, London
    Ib. (June 2001) [1909]. Ib. Part 2. 1815–1865. Waterloo to the Death of Leopold I. Ib. (Paperback 462pp ed.). Ib. ISBN 1-4021-6713-X.  Facsimile reprint of a 1909 edition by the author, London
  • Fitzmaurice, John (1996). The Politics of Belgium: A Unique Federalism. Nations of the modern world (Paperback 284pp ed.). Westview Press, Boulder, Colorado, USA. ISBN 0-8133-2386-X. OCLC 30112536. 
  • Kossmann-Putto, Johanna A.; Kossmann Ernst H.; Deleu Jozef H. M., ed.; Fenoulhet Jane, translator (from: (1987)). De Lage Landen: geschiedenis van de Noordelijke en Zuidelijke Nederlanden. Vlaams-Nederlandse Stichting Ons Erfdeel, Rekkem (January 1993) [1987]. The Low Countries: History of the Northern and Southern Netherlands (3rd Rev. edition Paperback 64pp ed.). Flemish-Netherlands Foundation "Stichting Ons Erfdeel", Rekkem, Belgium. ISBN 90-70831-20-1.  (Several editions in English, incl. (1997) 7th ed.)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ubelgiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.