Bata mzamaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bata mzamaji
Bata kichwa-chekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na bata)
Nusufamilia: Aythyinae
Ngazi za chini

Jenasi 4:

Mabata wazamaji ni ndege wa maji wa nusufamilia Aythyinae katika familia Anatidae. Spishi hizi huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji. Miguu yao iko nyuma zaidi ya mwili kuliko miguu ya mabata wachovya ili kujisogeza mbele vizuri ndani ya maji. Kwa sababu hiyo hawawezi kutembea vizuri. Hutokea kwa makundi kwa maji baridi au milango ya mito, lakini bata mzamaji mkubwa (Aythya marila) huingia bahari wakati wa majira ya baridi. Wanaweza kupuruka sana na spishi za kanda za kaskazini huhamia kusini kila majira ya baridi. Hujenga matago yao visiwani kwa maziwa au ndani ya uoto wa matete uliosongamana.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]