Bata bukini
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Bata bukini | ||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Mabata bukini ni ndege wakubwa wa maji wa familia ya Anatidae. Wanaainishwa katika familia ndogo Anserinae pamoja na mabata-maji. Mabata bukini ni ndege wakubwa sana lakini wadogo kuliko mabata-maji. Wana domo pana pia lakini shingo yao ni fupi zaidi. Wana rangi mbalimbali kama kahawia, nyeupe na nyeusi kadiri ya spishi. Hula mimea na pengine wadudu na nyungunyungu. Wanaweza kuwa wasumbufu wakiingia mashamba. Tago lao limejengwa kwa vijiti, manyasi n.k. karibu na maji na limetandikika na manyoya mororo.
Ndege hawa huzaana kwa kanda za kaskazini kabisa za dunia au juu sana ya milima. Spishi moja tu, Cereopsis novaehollandiae, huzaa katika nusudunia ya kusini na inaainishwa pengine katika familia ndogo yake mwenyewe. Wakati wa majira ya baridi mabata bukini huhama kanda za moto zaidi. Bata bukini hufugwa mahali pengi pa Afrika, lakini ndege mwitu hutokea tu kwa idadi kubwa huko Maroko, Aljeria na Tunesia wakati wa majira ya baridi ya Ulaya. Ndege wanaofugwa katika Afrika chini ya Sahara wanatokana aghalabu na bata bukini wa Uchina. Aina kadha zinatoka uzalishaji mtambuka wa mabata bukini wa Ulaya na Uchina.
[hariri] Spishi za Afrika
- Anser anser, Bata Bukini wa Ulaya (Greylag Goose)
- Anser anser domesticus (Domesticated goose)
- Anser cygnoides, Bata Bukini wa Uchina (Swan Goose) haitokei mwituni kwa Afrika
- Anser cygnoides domesticus (Chinese and African Goose)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Anser albifrons White-fronted Goose)
- Anser a. albifrons (Eurasian White-fronted Goose)
- Anser a. elgasi (Tule Goose)
- Anser a. flavirostris (Greenland White-fronted Goose)
- Anser a. frontalis (Pacific White-fronted Goose)
- Anser a. gambeli (Gambel White-fronted Goose)
- Anser brachyrhynchus (Pink-footed Goose)
- Anser cygnoides (Swan Goose)
- Anser erythropus (Lesser White-fronted Goose)
- Anser fabalis (Bean Goose)
- Anser f. fabalis (Western Bean Goose)
- Anser f. johanseni (Johansen Bean Goose)
- Anser f. middendorffi (Middendorf's Bean Goose)
- Anser f. rossicus (Russian Bean Goose)
- Anser f. serrirostris (Thick-billed Bean Goose)
- Anser indicus (Bar-headed Goose)
- Branta bernicla Brent Goose)
- Branta b. bernicla (Dark-bellied Brent Goose)
- Branta b. hrota (Pale-bellied Brent Goose)
- Branta b. nigricans (Black Brant)
- Branta canadensis Canada Goose)
- Branta hutchinsii (Cackling Goose) - zamani iliainishwa katika B. canadensis
- Branta hylobadistes (Nēnē-nui au Woods-walking Goose) kabla ya historia
- Branta leucopsis (Barnacle Goose)
- Branta ruficollis (Red-breasted Goose)
- Branta sandvicensis (Hawaiian Goose au Nēnē)
- Cereopsis novaehollandiae (Cape Barren Goose) pengine inaainishwa katika familia ndogo Cereopsinae
- Chen caerulescens (Snow Goose)
- Chen canagica (Emperor Goose)
- Chen rossii (Ross's Goose)