Banguko
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Banguko la mawe lililoharibu kijiji Puero Rico
Banguko ni kiasi kikubwa cha mawe, ardhi, theluji au barafu kinachoanza kusogea kwenye mtelemko wa mlimani na kuteleza au kuanguka kwa kuelekea bondeni.
Mwendo wa masi kubwa inaweza kusukuma miamba, miti na chochote kilichopo njiani kwenye mtelemko wa mlima na kuongeza banguko.
Banguko ni hatari kwa watu waliopo mlimani na pia kwa vijiji bondeni ambavyo vinafikiwa na banguko kubwa.
Katika Alpi za Ulaya takriban watu 100 hufariki kila mwaka kutokana na banguko.
Kwenye Andes za Peru watu 4,000 waliuawa na banguko kubwa tar. 11 Januari 1962. Banguko ya theluji ilitelemka mlima Huascaran na kufunika mji wa Yungay; mengine yalianguka katika mto na kusababisha mafuriko.