Bangladesh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bangla Desh)
Rukia: urambazaji, tafuta
গণপ্রজাতন্ত্রী বাংলােদশ
Gônoprojatontri Bangladesh

Jamhuri ya Watu wa Bangladesh
Bendera ya Bangla Desh Nembo ya Bangla Desh
Bendera Nembo
Wito la taifa:
Wimbo wa taifa: Amar Shonar Bangla
"Bengali yangu ya dhahabu"
Lokeshen ya Bangla Desh
Mji mkuu Dhaka
23°42′ N 90°22′ E
Mji mkubwa nchini Dhaka
Lugha rasmi Kibengali (Bangla)
Serikali Jamhuri
Zillur Rahman
Sheikh Hasina Wajed
Uhuru
Ilitangazwa
Siku ya Ushindi
26 Machi 1971
16 Desemba 1971
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
144,000 km² (ya 94)
7.0
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
147,365,352 (ya 7)
129,247,233
998.6[1]/km² (ya 7)
Fedha Taka (BDT)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
BDT (UTC+6)
not observed (UTC+6)
Intaneti TLD .bd
Kodi ya simu +880 - SubCodes

-



Bangladesh (pia: Bangla Desh; Kibengali: বাংলাদেশ, bāṃlādeś) ni nchi ya Asia ya Kusini. Imepakana na Uhindi pande zote barani isipokuwa mpaka mfupi wa 193 km na Myanmar upande wa kusini-mashariki na pwani la Ghuba ya Bengali.

Bangladesh ni sehemu ya mashariki ya Bengali ya kihistoria iliyotenganishwa wakati wa mgawanyiko wa Uhindi kwa sababu wakazi wake walikuwa Waislamu tofauti na Wabengali wengine Wahindu.

Baada ya mgawanyiko wa Uhindi Bangladesh ilikuwa sehemu ya Pakistan ikaitwa "Pakistan ya Mashariki" hadi 1971 ilipojitenga kutoka Pakistan kwa msaada wa India katika Vita ya Uhuru ya Bangla Desh.

Sehemu kubwa ya nchi ni delta ya mito Ganga na Brahmaputra. Uso wa nchi ni tambarare na mita chache tu juu ya uwiano wa bahari. Hivyo wananchi huteseka mara nyingi na mafuriko makali.

Marejeo [hariri]

  1. World Bank Development Indicators Database, 2006.

Viungo vya nje [hariri]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bangladesh kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.