Bandar Abbas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makao makuu ya Mkoa wa Hormozgan (Bandar Abbas)



Bandar Abbas
Majiranukta: 27°11′10″N 56°17′30″E / 27.18611°N 56.29167°E / 27.18611; 56.29167
Nchi Uajemi
Majimbo Hormozgan
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 352,173

Bandar Abbas (Farsi بندر عباس) ni makao makauu ya mkoa wa Hormozgan katika Uajemi. Ni mji wa bandari kwenye pwani la Mlango wa Hormuz wa Bahari Hindi. Mji ni kati ya mabandari muhimu ya nchi. Pia ni kituo muhimu cha jeshi la wanamaji la Uajemi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Bandar Abbas imetandazwa mita chache juu ya uwiano wa Bahari kwenye pwani la bahari.

Hali ya hewa ni la joto na unyevu anga kubwa wakati wa miezi Mei hadi Septemba na halijoto inafikia sentigredi 49. Miezi ya Novemba hadi Aprili yanapendeza hakuna joto kali na watu kutoka nyanda za juu za Uajemi wanafika hapa kwa likizo.

Usimbisaji karibu wote hutokea katika miezi ya Desemba hadi Aprili. Kwa wastani kuna usimbisaji wa milimita 251 kwa mwaka na unyevuanga kwa wastani 66 %.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la Bandar Abbas lilkuwa na miji na vijiji mbalimbali katika historia vilivyoenea katika eneo la mji wa leo.

Habari za kwanza ziko kutoka enzi la mfalme Darius I aliyetuma meli kwneda Uhindi kutoka hapa. Baadaye ni jeshi la Aleksander Mkuu lililopita hapa mnamo mwaka 325 KK wakati wa kurudi kutoka Uhindi.

Katika karne ya 16 Wareno walifika hapa waliotwaa kisiwa cha Hormus na kutumia pwani kama chanzo cha vyakula. Baada ya mwaka 1600 Wareno walifukuzwa kwa ushrikiano wa Uingereza na serikali ya Shah Abbas I aliyeagiza kujenga mji upya na kuupa jina lake yaani Bandar Abbas (bandari ya Abbas).

Baada ya kudhoofika kwa utawala wa nasaba ya Safawi hali ya mji ilishuka tena. Katika karne ya 20 ni hasa kujengwa kwa reli na bandari mpya kulikoweka msingi kwa ufufuo wa kiuchumi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.