Bahari ya Kaspi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bahari ya Kaspi kutoka angani.
Stenka Razin (Vasily Surikov)

Bahari ya Kaspi (pia: Bahari ya Qazwin; kwa Kiajemi: دريا خزر "darya khazar"; kwa Kirusi: Каспийское море "kaspiiskoye more") ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371,000 na mjao wa km³ 78,200. Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.

Kimo chake kinafikia mita 1,025.

Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.

Maji ya chumvi[hariri | hariri chanzo]

Upande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.

Madini[hariri | hariri chanzo]

Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi, hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]