Atanasi Bazzekuketta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Atanasi Bazzekuketta (1866 - Nakivubo 27 Mei 1886) ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.

Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 27 Mei[1].

Siku hiyo, wakati wa kupelekwa kuuawa pamoja na wenzake, aliwaomba watesi wammalize haraka, nao wakampiga fimbo hadi kufa. Alikuwa amebatizwa tangu muda mfupi tu[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.