Ashgabat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ashgabat عشق آبادا Ашхабад

Kitovu cha Ashgabad pamoja na sanamu ya Turkmenbashi (Turkmenistan)
Habari za kimsingi
Mkoa Eneo la mji mkuu Ashgabad (Aşgabat şäheri)
Anwani ya kijiografia Latitudo: 37°58′N - Longitudo: 58°20′E
Kimo 230 m juu ya UB
Eneo 488 km²
Wakazi 695,300 (2001)
Msongamano wa watu watu 1,424 kwa km²
Simu +993 (nchi), 12 (mji)
Mahali

Ashgabat (Kiturkmeni: Aşgabat; Kiajemi: عشق آباد; Kirusi: Ашхабад) ni mji mkuu wa Turkmenistan pia mji mkubwa wa nchi hii mwenye wakazi 695,300 (2001). Jina laandikwa pia Ashghabat, Ashkabat au Ashkhabad kwa mwandiko wa kilatini.

Mji uko katika oasisi ya jangwa la Karakum mguuni wa milima ya Kopetdag karibu na mpaka wa Uajemi.

Mji una viwanda vingi vya machine, vifaa vya umeme, nguo na chakula. Kuna pia vyuo na shule nyingi.

Kati ya wakazi kuna Waturkmeni, Warusi, Waarmenia na Waazeri. Walio wengi ni Waislamu Wasunni lakini kuna pia Wakristo na Baha'i

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Ashgabat ulikua kutoka kituo cha kijeshi cha Urusi. Tangu 1885 uliunganishwa kwa reli na majimbo mengine ya Asia ya Kati ukaanza kukua. Kati ya 1919 hadi 1927 mji ukaitwa "Poltorazk".

1924 ulikuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiturkmeni ndani ya Umoja wa Kisovyeti. Ashgabat iliharibika katika tetemeko la ardhi tar. 5 Oktoba 1948 na kujengwa upya.

Wakati wa uhuru wa Turkmenistan tar. 27 Oktoba 1991 Ashgabat imekuwa mji mkuu wa nchi huru.

Picha za Ashgabad[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ashgabat kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.