Amos Biwott

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Olympic medal record
Riadha ya Wanaume
Dhahabu 1968 Mexico City Mbio ya 3000 m ya urukaji wa viunzi

Historia[hariri | hariri chanzo]

Amos Biwott (alizaliwa 8 Septemba 1947 katika Wilaya ya Nandi) ni mwanariadha wa zamani wa Kenya. Yeye alikuwa mshindi wa mbio ya 3000m ya urukaji viunzi katika Olimpiki ya 1968.

Alizaliwa katika eneo la Nandi, Kenya. Amos Biwott alikuwa wa kwanza katika orodha refu ya wanariadha wa Kenya waliomfuata na kushiriki katika mbio ya 3000m ya urukaji viunzi. Tangu kushinda mbio hiyo ,kwa njia ya kiajabu, katika michezo ya Olimpiki ya Mexico City, Biwott alifungulia Waafrika wengine njia katika kushinda mbio za masafa marefu.

Biwott hakuwa amekimbia mbio nyingi za urukaji viunzi kabla ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki hiyo, alikuwa amekimbia mbio tatu tu. Hivyo basi, mtindo wake haukuwa bora na wa kawaida hasa katika kuruka viunzi. Alitumia njia ya iliyochekesha sana. Alikuwa mtu wa kwanza kuwa na ujasiri wa kuruka kikwazo chote bila kukikanyaga, mbinu hii ilihitaji kuruka kwa nguvu kwelikweli. Alipotumia mbinu hiyo ya kuruka hivyo, alipunguza muda wa kuruka viunzi (uliokuwa sekunde 1.1) kwa nusu ukawa sekunde 0.55. Yeye ndiye alikuwa mwanariadha pekee kumaliza mbio hiyo na miguu kavu bila maji hata kidogo katika mbio ya uhitimu na hata katika fainali. Alishinda mbio ya fainali akiwa mbele ya mwanariadha mwenzake kutoka Kenya , Benjamin Kogo. Alimshindia muda wa sekunde 0.6.

Baada ya kushinda mbio hizi, Biwott alianza kufeli katika mbio zake. Alichukua nafasi ya tatu katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1970 , akawa nambari sita katika Olimpiki ya 1972 na akamaliza mbio yake ya mwisho akiwa nafasi ya nane katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1974.

Baada ya kufeli katika riadha, Biwott alifanya kazi katika Idara ya Kenya Prisons mpaka alipotoka huko katika mwaka wa 1978 aliposhtakiwa kwa wizi. Baadaye, akawa bawabu wa uwanja wa mazoezi.

Alimwoa Cherono Maiyo, aliyeshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya 1972 akawa mmojawapo wa wanawake wa Kenya wa kwanza kushiriki katika Michezo ya Olimpiki. Walifunga ndoa katika mwaka wa 1973 na wana watoto watano.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]