Amazonas (mto)
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Mto wa Amazonas | |
|---|---|
|
|
|
| Chanzo | mlima Nevado Mismi (Peru) |
| Mdomo | Atlantiki |
| Nchi | Brazil (62.4%), Peru (16.3%) Bolivia (12.0%), Kolombia (6.3%) Ekuador (2.1%) |
| Urefu | 6,400 km |
| Kimo cha chanzo | takriban 5,597 m |
| Tawimito upande wa kulia | Purus, Madeira, Tapajós, Xingu, Tocantins |
| Tawimito upande wa kushoto | Marañón, Japurá, Rio Negro |
| Mkondo | 219,000 m³/s |
| Eneo la beseni | 6,915,000 km² |
| Miji mikubwa kando lake | Manaus, Macapa, Santarem |
Mto Amazonas (Kireno: Rio Amazonas) ni mto mkubwa duniani. Ina chanzo chake katika milima ya Andes inavuka beseni yake hadi Atlantiki kupitia eneo kubwa la misitu minene. Sehemu kubwa ya mwendo wake iko katika nchi ya Brazil. Inabeba maji zaidi kuliko mito ya Nile, Mississippi na Yangtse pamoja.
Kuhusu urefu hakuna mapatano bado kama Nile au Amazonas ni mto mrefu duniani. Makadirio hutegemea ni tawimto upi mwenye chanzo cha mbali zaidi unaokubaliwa na wataalamu. 1969 urefu wake ulipimwa kuwa 6.400 km.[1]
Amazonas ina tawimito zaidi ya 10,000 na kati ya hizi kuna 17 zenye urefu wa zaidi ya 1,600 km zikishinda mito kama Senegal, Gambia au Nile ya buluu.
Upana wa mto ni wa kilomita kadhaa kufika hadi 100 km wakati wa mafuriko ya kila mwaka. Delta ya Amazonas ina upana wa mamia ya kilomita; ndani yake kuna kisiwa cha Marajó chenye eneo la 49,000 km² ambalo ni kubwa kushinda nchi kama Rwanda au Burundi.
Amazonas ni njia muhimu ya mawasiliano na usafiri nchini Brazil. Meli kubwa za baharini zinaweza kuingia hadi bandari ya Manaus iliyoko 800 km ndani ya bara. Meli ndogo za baharini hadi uzito wa tani 3,000 zinaweza kuvuka Brazil yote na kufika Peru.
[hariri] Viungo vya Nje
- Amazon River and Amazon Rainforest virtual tour
- Information on the Amazon from Extreme Science
- Map of South America
- Pictures of the Amazon River
- Amazon River and rainforest photos and information
- An Amazon River web site
- Information and a map of the Amazon's watershed
| Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Amazonas (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |