Amani Temba
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Amani James Pausen Temba |
|
|---|---|
|
|
|
| Jina la Kiraia | Amani James Pausen Temba |
| Jina la kisanii | Mheshimiwa Temba |
| Nchi | Tanzania |
| Alizaliwa | 1980 |
| Aina ya muziki | Hip Hop na Bongo Flava |
| Kazi yake | Mwanamuziki, Mchezaji Mpira wa Kikapu |
| Miaka ya kazi | mn. 1999 - |
| Ameshirikiana na | Dully Sykes, Ray C nk. |
| Ala | Muimbaji |
| Kampuni | Bongo Records, Mandugu Digital |
Amani James Pausen Temba au "Mheshimiwa Temba" (kifupi Mh Temba) ni Mwanamuziki wa Rap na Hip Hop Kutoka Jijini Dar es Salaam Tanzania, Na pia ni Mwanachama Kiongozi wa Tmk Wanaume Family yenye makazi yao huko Temeke Jijini Dar es Salaam Tanzania, Mh Temba alizaliwa mwaka 1980 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Temeke na baadaye kujiunga na shule ya sekondari ya Nuru Yakini ambako alisoma kwa miaka miwili kabla ya kuhamia sekondari ya Makongo, alisoma Makongo kwa mda wiki moja tu na kwenda kujiunga na sekondari nyingine inayomilikiwa na Jeshi ya Jigetemee baada ya kupata ofa ya kusomeshwa bure na uongozi wa shule hiyo enzi hizo ukiwa chini ya Luteni kanali Fabian Massawe ambaye sasa ni Mkuu wa wilaya ya kinondoni.
[hariri] Maisha ya Muziki
Mwanzoni alitokea kwenye kundi flani liitwalo "Manduli Mobb" walifanya nyimbo kadha wa kadha ikiwemo ile ya 'Maskini Jeuri' walishirikiana na 'Juma Nature' hiyo ilikuwa mwaka 2000 baadae kundi lika tawanyika na kila mtu kuanza kufanya kazi za muziki akiwa peke yake na sio na kundi tena, alio anza kutoa nyimbo yake peke alikuwa "Bwana Mkubwa" baadae Mh Temba nae akatoa nyimbo yake ya kwanza ilioitwa "Nakumaindi" ilikuwa mwaka 2001 Mwishoni ambayo ilitayarishwa na Muuandaaji Papa Lavu maarufu kama Bonny Lavu.
miaka iliyo fuatia akajiunga na Tmk Wanaume enzi hizo 'Juma Nature ajatoka kwenye kundi la Tmk Wanaume Mh Temba akatoa nyimbo nyingine iliyoitwa "Nampenda Yeye" ambayo aliimba na Dully Sykes nayo ilivuma sana na kumpa heshima kubwa katika medani ya Muziki Tanzania baadae akawa anapata ushirika mwingi tu na wasanii mbali mbali.

