Alhamisi kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Karamu ya Kiroho ilivyochorwa na Simon Ushakov (1685).
"Karamu ya mwisho" ilivyonakiliwa kutokana na kazi ya mchongaji Master Paul.
Picha ya Kiorthodoksi ya Kristo kuwaosha miguu Mitume (karne ya 16, shule ya uchoraji ya Pskov).

Alhamisi kuu ni sikukuu ya Ukristo inayoadhimisha jioni ile karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake kabla hajakamatwa na kuhani mkuu wa Israeli, Yosefu Kayafa.

Katika karamu hiyo Yesu alitoa maneno yake ya buriani kwa wanafunzi hao akikazia amri mpya ya kwamba wapendane jinsi yeye alivyowapenda upeo, inavyosimuliwa hasa katika Injili ya Yohane.

Umuhimu wa tukio hilo unasisitizwa hasa na madhehebu yanayoamini kuwa ndipo Yesu Kristo alipoweka sakramenti ya ekaristi (na ya upadri), inavyosimuliwa katika Injili nyingine tatu.

Tarehe ya adhimisho hilo inabadilikabadilika pamoja na ile ya Pasaka, lakini inaangukia kati ya tarehe 19 Machi na 22 Aprili, lakini kwa Waorthodoksi wanaofuata kalenda ya Juliasi tarehe hizo ni sawa na tarehe 1 Aprili na 5 Mei ya kalenda ya kawaida.

Adhimisho la karamu ya mwisho, ambalo kwa kawaida linaendana na kutawadha miguu ya wanaume 12 kwa kuiga tendo la Yesu, ndio mwanzo wa siku tatu kuu za Pasaka ambazo kilele chake ni kesha la usiku wa Pasaka, Yesu anaposadikiwa kuwa amefufuka.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]