Alexander wa Lyon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Alexander wa Lyon ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Lyon wanaoheshimiwa kama watakatifu. Inasemekana alikuwa mganga kutoka Frigia (katika Uturuki wa leo).

Ni kwamba mwaka 177 dhuluma ya kaisari Marcus Aurelius dhidi ya Ukristo ilisababisha mauaji makubwa katika mji mkuu wa Gallia, jina lake Lyon.

Kati yao, ni maarufu hasa askofu Potinus wa Lyon na bikira Blandina wa Lyon. Wengine ni huyo Alexander, halafu Attalus wa Lyon, Espagathus wa Lyon, Maturus wa Lyon, na Sanctius wa Lyon.