Aleksander Mashuhuri
| Aleksander Mashuhuri (Mkuu) | |
|---|---|
| Mfalme wa Masedonia | |
| Aleksander jinsi alivyomshambulia mfalme Dario wa Uajemi kwenye mapigano ya Issos(mozaiki ya Aleksander mjini Napoli, Italia) | |
| Kusimikwa | 336 |
| Vyeo vingine | Mkuu wa shirikisho la Wagiriki, Shahansha wa Uajemi, Farao wa Misri, Bwana wa Asia |
| . | |
| Wake | Roksana wa Baktria Stateira wa Uajemi Parysatis wa Uajemi |
| Nasaba | Nasaba ya Masedonia |
| Baba | Filipo II wa Masedonia |
| Mama | Olimpia wa Epiros |
Aleksander Mashuhuri (au Aleksanda Mkuu, kwa Kigiriki Μέγας Αλέξανδρος, inayoandikwa kwa alfabeti yetu Megas Aleksandros) aliishi tangu Julai 356 KK hadi tarehe 11 Juni 323 KK.
Mfalme wa Masedonia (336 – 323 KK), anajulikana kama mmoja kati ya amiri jeshi waliofanikiwa kupita wote wengine katika historia ya dunia. Kabla hajafariki bado kijana aliteka sehemu kubwa ya dunia iliyojulikana na Wagiriki wa zamani zake, kuanzia Ulaya mashariki kusini hadi India na Misri.
Mitazamo juu yake [hariri]
Katika Deuterokanoni anatajwa na vitabu vya Wamakabayo kama mwanzilishi wa dola lililoeneza ustaarabu wa Kigiriki hata kuhatarisha imani ya Wayahudi na kuwadhulumu wakati wa mwandamizi wake Antioko Epifane wa Syria.
Katika kitabu cha Kizoroastria cha kipindi cha kati ya Uajemi kilichoitwa Arda Wiraz Nāmag Aleksander anajulikana kama “Aleksander aliyelaaniwa” kwa sababu alishinda milki ya Uajemi na aliangamiza mji mkuu wake ulioitwa Persepolis. Lakini katika habari za baadaye za Uajemi, mpaka Irani ya siku hizi, anaitwa Eskandar na hata alishangiliwa wakati Ukuta Mkuu wa Sadd-e Eskandar ulijengwa wakati wa Ufalme wa Parthia.
Pia anajulikana katika desturi za Mashariki ya Kati kama Dhul-Qarnayn kwa Kiarabu na Dul-Qarnayim kwa Kiyahudi na Kiaramu, yaani "mtu mwenye pembe mbili", huenda kwa sababu picha kwenye sarafu za wakati wa utawala wake ilimwonyesha kama anazo pembe mbili za kondoo dume za mungu Ammon wa Misri.
Jina lake kwa Kihindi ni Sikandar, neno ambalo ni sawa na “mtaalamu” au “mtu stadi.”
| Makala hii kuhusu mtu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Aleksander Mashuhuri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |