Alberto wa Pisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alberto wa Pisa alivyochorwa.

Alberto wa Pisa, padri wa Kanisa Katoliki kutoka Pisa (Italia), alikuwa mkuu wa tatu wa shirika la Ndugu Wadogo (badala ya Elia Bombarone) tangu mwaka 1239 hadi alipofariki mwaka 1240.

Kabla ya hapo aliwahi kuwa mkuu wa kanda ya shirika huko Ujerumani na Hungaria, akashika nafasi ya Agnellus wa Pisa kama mkuu wa kanda ya Uingereza, kanda ambayo kuliko zote ilikua mbali na Fransisko wa Asizi na kujali elimu.[1].

Ingawa alifariki baada ya miezi michache tu, uchaguzi wake ulionyesha kwamba maendeleo ya shirika, yaliyotakiwa na viongozi wa Kanisa na ndugu walio wengi, yataanza tena kusonga mbele moja kwa moja.

Kwamba maendeleo hayo yalikuwa kinyume cha nia asili ya mwanzilishi (walivyosisitiza wenzake na wengineo waliomfahamu vizuri) haikuwa kizuio kwa umati walioridhika tu kutekeleza amri za kanuni, kuwa fukara kuliko watawa wengine na kuheshimiwa na waamini pia kwa niaba ya mzee wao aliyezidi kutazamwa mkuu ajabu.

Baada yake akachaguliwa Aimoni wa Faversham (1240-1244), Mwingereza mwanateolojia aliyekuwa ameongoza upinzani dhidi ya Elia Bombarone.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Padre Pio The Franciscan - Order of Friars Minor". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-14. Iliwekwa mnamo 2011-02-15. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]