Akida Korneli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Petro Akimbatiza Akida Korneli, kadiri ya Francesco Trevisani, 1709.

Akida Korneli (kwa Kigiriki, Κορνήλιος, Kornelios) alikuwa akida wa kikosi cha Italia katika jeshi la Dola la Roma aliyefanya kazi huko Kaisarea Baharini (Palestina). Huko alivutiwa na dini ya Uyahudi hata akajitolea kujenga sinagogi, pamoja na kusali.

Wongofu wake na wa jamaa zake unasimuliwa mara tatu na Matendo ya Mitume kwa jinsi ulivyotiwa maanani na Luka mwinjili aliyetaka kueleza kwamba desturi ya kubatiza watu wa mataifa bila kudai kwanza watahiriwe ilianzisha na Mtume Petro kwa kuangazwa na Mungu.

Suala hilo lilisumbua sana Kanisa la mwanzo hata baada ya Mtaguso wa Yerusalemu (49 BK) kupitisha desturi hiyo (Mdo 15).

Baada ya kuongoka, inasimuliwa kwamba alishuhudia Injili hadi Misia (leo nchini Uturuki) akateswa kwa ajili hiyo.

Habari nyingine zinasema alipata kuwa askofu na nyingine alifia dini.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Oktoba[1][2] lakini pia 13 Septemba au 2 Februari.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akida Korneli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.