Afrika
Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa mraba 30,244,050 na wakazi bilioni 1 (mwaka 2009). Asia ndiyo bara pekee kubwa kushinda Afrika.
Yaliyomo |
Jina la Afrika
Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.
Lugha
tazama makala "Lugha za Afrika"
Zaidi ya lugha elfu za Kiafrika zinazungumzwa katika Afrika leo.
Lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili) ni lugha muhimu katika Afrika ya Kusini, Afrika ya Kati na Afrika ya Mashariki.
Kiarabu ni lugha muhimu Afrika ya Kaskazini.
Lugha za Ulaya zinazumgumzwa pia, hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno.
Kiafrikaans ni lugha ya pekee ya Afrika Kusini yenye asili ya Ulaya.
Nchi za Afrika
Tazama makala "Orodha ya nchi za Afrika
Vitabu
- History of Africa Marco Notari, for Africa
- Maria Petringa. Brazza, A Life for Africa, 2006. ISBN 978-1-4259-1198-0.
Tazamia pia
