Adowa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adowa (pia: Adwa, Adua) ni mji wa Ethiopia karibu na mpaka wa Eritrea. Mwaka 2005 ulikuwa na wakazi 43,582. Adowa ni sehemu ya mkoa wa Tigray katika nyanda za juu za Ethiopia kwa kimo cha mita 1,900.
[hariri] Historia
Adowa ni mji wa kale imetajwa mara ya kwanza katika kumbukumbu ya kimaandishi wakati kundi la Wareno lilipopita hapa mwaka 1520. Baadaye ilikuwa mji muhimu iliyotawala njia za kuingia nyanda za juu kutoka pwani la Bahari ya Shamu na mnamo 1700 ikawa makao makuu ya gavana ya Negus kwa jimbo la Tigray.
Adowa ilijulikana hasa kimatifa kutokana na mapigano ya Adowa ambako jeshi la Negus Menelik II ilishinda uvamizi wa Waitalia chini ya jenerali Oreste Baratieri. Ushindi huu ulizuia jaribio la Italia kuifanya Ethiopia kuwa koloni yake ikahakikisha uhuru wa Ethiopia.