Abushiri ibn Salim al-Harthi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya Pangani na pwani la Tanzania mnamo 1889.
Alikuwa mfanyabiashara na mwenye shamba ya miwa karibu na Pangani. Agosti 1889 aliongoza upinzani dhidi ya utawala wa Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki katika eneo la Pangani.
Baada ya miezi ya mapambano ( taz. vita ya Abushiri) alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani tarehe 16 Desemba 1889.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abushiri ibn Salim al-Harthi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |