Kitabu cha Kwanza cha Wafalme

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka 1Fal)

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 22.

Historia ya kitabu[hariri | hariri chanzo]

Zamani kilikuwa kitabu kimoja na Wafalme II lakini katika tafsiri ya Septuaginta kitabu kiligawiwa pande mbili. Wataalamu huamini hii ilitokea kutokana na urefu wa kitabu, si kwa sababu ya yaliyomo au ya mpangilio wake.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yaliyomo[hariri | hariri chanzo]

Kinasimulia hasa habari za wafalme wa Israeli ya Kale. Chanzo ni habari za kifo cha mfalme mzee Daudi na hasa za mwanae Solomoni aliyemfuata madarakani. Kina pia maelezo kuhusu ujenzi wa hekalu la Yerusalemu.

Kinachofuata ni habari za ugawaji wa milki kuwa madola mawili yaani:

Habari za nabii Eliya na nabii Elisha pia zinapatikana humo.

Kati ya masimulizi mashuhuri sana ya kitabu hiki ni hukumu aliyotoa Suleimani kuhusu makahaba wawili kugombania mtoto mchanga (Wafalme I 3, 16-27).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Kwanza cha Wafalme kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.